BUKOBA SPORTS

Sunday, June 24, 2012

MABINGWA WATETEZI HISPANIA WATINGA NUSU FAINALI YA UERO 2012 KWA KISHINDO WAIFUNGA UFARANSA BAO 2-0

  Mabingwa watetezi wa Euro 2012 waliweza kuishinda Ufaransa magoli 2-0, timu ambayo wakati mwingine ilionyesha ustadi wao katika mchezo, lakini kwa jumla wakiwa dhaifu na kukosa mbinu walipolifikia lango la wapinzani wao.
Uhispania, baada ya ushindi huo katika uwanja wa Donetsk usiku wa Jumamosi, sasa itakutana na Ureno katika mechi ya nusu fainali.
Jordi Alba, kwa haraka haraka alifanikiwa kumchenga mlinzi aliyemuandama na kuupiga mpira juujuu, na ambao ulimfikia Xabi Alonso, ambaye pasipo kusita alikuwa ameusubiri kwa makini, na kuusindikiza kwa kichwa hadi wavuni, akiandikisha bao la Uhispania baada ya dakika ya 20 za mchezo.

Kwa kawaida Xabi Alonso huwa hakosi kufunga mikwaju ya penalti inapojitokeza, na katika dakika ya 91, aliweza kufunga bao la pili, na akiuelekeza mpira hadi kona ya lango.
Kwa mbinu hafifu Ufaransa ilijitahidi kuitisha Uhispania, lakini juhudi zao za pekee zilizokaribia kuandikisha bao ni wakati Mathieu Debuchy alipousindikiza mpira kwa kichwa kuelekea wavuni baada ya kupigiwa mpira na Franck Ribery.Mashabiki wa spain wakishangilia uwanjani
Another victory: Spain boss Vicente Del Bosque encourages his team
Bosi wa spain Vicente Del Bosque akisisitiza jambo kuwa waendeleze mashambulizi goli moja halitoshi..
Plenty to ponder: It wasn't a night to remember for France coach Laurent Blanc
Kocha wa Ufaransa Laurent Blanc akisikilizia moyo na kukumbuka kilichowahi kuwapata hapo nyuma


Battle: Adil Rami challenges Spain's Cesc Fabregas
Adil Rami akichuana na Cesc Fabregas

On the run: Spain pair Gerard Pique and Alvaro Arbeloa try to keep up with Franck Ribery
My ball: France goalkeeper Hugo Lloris makes a save in front of Fabregas
Hapa  Hugo Lloris alidaka mpira uliopigwa na  Fabregas
Going close: Fance goalkeeper Lloris saves from Spain substitute Fernando Torres
Golikipa wa Ufaransa Lloris akijaribu kuokoa mpira kutoka kwa Fernando Torres
 Samir Nasri akimpongeza Jesus Navas mchezaji wa Spain baada ya mtanange kuisha

No comments:

Post a Comment