BUKOBA SPORTS

Thursday, June 7, 2012

MAN UNITED KUTOA OFA YA PAUNI MILIONI 22 ILI KUNYAKUWA LUKA MODRIC WA SPURS!

Kuna taarifa kuwa Manchester United wanatayarisha ofa ya Pauni Milioni 22 ili kumnunua Kiungo wa Tottenham Luka Modric.
Man United tayari wamekubaliana na Borussia Dortmund ili kumchukua Nyota wa Japan Shinji Kagawa ambaye uhamisho wake KUMNASA MODRIC utakamilika baadaye Mwezi huu baada ya Mchezaji huyo kufuzu upimaji afya na kupata Kibali cha Kazi cha Uingereza.
 
Hivi juzi Sir Alex Ferguson aliripotiwa kugwaya dau la Pauni Milioni 32 wanalotaka Tottenham kwa Modric, Miaka 26, lakini ofa hii ya Pauni Milioni 22 inaelekea ni kufungua mazungumzo kuhusu uhamisho huu wa Staa huyo wa Croatia.
Mwaka jana, Chelsea walimwania Modric lakini Tottenham wakagoma kumuuza lakini safari hii kukosa kwa Tottenham kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao huenda kukamfanya Modric atake kuhama.
Mbali ya Modric, Sir Alex Ferguson pia inasemekana anawawinda Kiungo wa Newcastle Cheick Tiote na Fulbeki wa Everton Leighton Baines ingawa hadi sasa kikwazo ni madau wanayotaka Klabu zao wakati Ferguson amesema pesa zinazotakiwa si thamani ya Wachezaji hao.
Wakati huo huo, Mchezaji kutoka Ghana anaechezea Udinese huko Italia, Kwadwo Asamoah, amedokeza yuko tayari kuhamia Ligi Kuu England na inaaminika lengo lake ni kuchezea Manchester United.

Kwadwo Asamoah (katikati) and Emmanuel Agyemang-Badu (kulia)
Asamoah ameposti kwenye Akaunti yake ya Mtandao wa Twitter akidai Wiki ijayo ndio kutatoka taarifa rasmi kuhusu uhamisho wake.
 

No comments:

Post a Comment