Manchester United imethibitisha kuwa itakwenda Afrika Kusini Mwezi ujao kucheza Mechi za kujipima nguvu na Klabu za huko AmaZulu FC Mjini Durban na Ajax Cape Town Mjini Cape Town ikiwa ni sehemu ya Ziara ya 2012 ambayo huandaliwa ili kuitayarisha Timu kwa ajili ya Msimu mpya wa Mwaka 2012/13 unaotarajiwa kuanza Agosti 18.
Nchi nyingine ambazo Man United watazuru kwa ajili ya Mechi ni China na Norway.
Manchester United = ZIARA 2012:
Julai 18= Amazulu FC (Moses Mabhida Stadium, Durban)
Julai 21= Ajax Cape Town (Cape Town Stadium)
Julai 25= Shanghai Shenhua (Shanghai Stadium, Shanghai - China Cup)
Agosti 5= Valerenga (Ullevaal Stadium, Oslo, Norway)
Mechi hizo mbili za huko Afrika Kusini zitadhaminiwa na MTN, Kampuni ya Simu za Mkononi ambao pia ni Wadhamini wa Man United Nchini Afrika Kusini na Mechi ya huko Durban itakuwa moja ya kilele cha kuitukuza Siku ya Mandela ambayo husheherekewa Julai 18.
Manchester United walishawahi kuzuru Afrika Kusini mara mbili Mwaka 2006 na 2008.
No comments:
Post a Comment