BUKOBA SPORTS

Thursday, June 7, 2012

CHRISTIAN RONALDO: NATAKA KUCHEZEA REAL MADRID MAISHA YANGU YOTE

Mchezaji huyo ambaye alijiunga na real madrid kwa ada ya kutisha ya Paundi milioni 80 amesema anataka kuendelea kukipiga katika klabu hiyo kwa maisha yake yote yaliyobaki katika soka na kuondoa uvumi kwamba mchezaji huyo alikuwa na uwezekano wa kurudi manchester united na pia kuondoa uvumi uenda akahitajika na Manchester city.

 Mchezaji huyo ambaye anajiandaa na mashindano ya ulaya yanayotarajiwa kuanza weekend ijayo ameifungia timu yake ya real madrid mabao 60 msimu uliopita na kuiwezesha kunyakua ubingwa wa Hispania.

Ningepewa mamlaka ya kuamua ningeamua kubaki real madrid kwa maisha yangu yote lakini siyo mimi mwenye maamuzi hayo, Siyo kama naongea tu bali naongea kutoka moyoni kwamngu kwamba naipenda real madrid na ningependa nimalizie soka langu nikiwa mahali hapa. Ningeweza kusaini mkataba wa miaka 10 lakini hiyo yote siyo juu yangu ni juu ya wote wanaofanya maamuzi katika timu ya real madrid.

Ronaldo alisema kwamba mambo yote niliyoyafanya hapa ni kutokana na juhudi zangu na kujituma hakuna kitu hata kimoja kimeshushwa kutoka angani. Nafurahi nimekuwa mchezaji ambaye nimesajiliwa kwa gharama kubwa sana na napenda kudhihirisha hilo nikiwa uwanjani nafanya vitu vyangu kwa kuwa iki ndicho ninachoweza kufanya kuonyesha fadhila zangu kwa klabu ambayo ilitumia mamilioni ya fedha kunileta hapa.

Jose mourinho amesaini mkataba mpya na real madrid, nimefurahi kwa sababu jose Mourinho ni kocha mzuri siyo kwa sababu yeye ni mreno kama mimi bali anajua anachokifanya na ni kocha ambaye anaweza kuwaunganisha wachezaji wote.

No comments:

Post a Comment