
picha mbalimbali wachezaji wa England wakiwasili katika jiji la Poland na kupokelewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki wao ambao walikuwa tayari wanawasubiri, wachezaji hao wamewasili katika Jiji hilo tayari kwa mashindano ya ulaya EURO 2012 ambayo yanatarajiwa kuanza kupigwa katika viwanja mbalimbali hapo kesho tarehe 08/06/2012

Leo, msafara wa England ukiongozwa na Meneja wao Roy Hodgson, umetua Nchini Poland tayari kwa Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa kwa pamoja Nchini Poland na Ukraine kuanzia Juni 8 na moja kwa moja wakaelekea Krakow kwenye Kambi yao.
No comments:
Post a Comment