BUKOBA SPORTS

Thursday, June 7, 2012

VIWANGO VYA FIFA UBORA DUNIANI: SPAIN IPO PALE PALE, TANZANIA YAPANDA NAFASI 6 NI YA 139

Spain ambayo ndiyo Mabingwa wa Ulaya na Dunia, watatinga Fainali za EURO 2012 wakiwa bado wanashikilia Nambari Wani kwenye Listi ya FIFA/Coca Cola ya Ubora Duniani iliyotolewa leo huku Tanzania ikipanda nafasi 6 na kushikilia Nambari 139.
Spain wanafuatiwa na Uruguay ambao wamewapiku Germany waliotupwa nafasi ya 3.

Timu zinazofuatia kwenye 10 Bora ni Netherlands, Brazil, England, Argentina, Croatia, Denmark na Portugal ambao wamedondoka nafasi 5.
Brazil, England, Argentina na Denmark zote zimepanda nafasi moja kila mmoja.
Kwa Bara la Afrika, Ivory Coast ndio iko juu ikishikilia nafasi ya 16 baada ya kuteleza nafasi moja na inafuatia Ghana walio nafasi ya 25, Algeria ni wa 32 na Libya wapo 42.
Mabingwa wa Afrika, Zambia, wao wapo nafasi ya 43, baada ya kuporomoka nafasi 3.
Listi nyingine ya Ubora itatolewa Julai 4.

No comments:

Post a Comment