Manchester United na Borussia Dortmund zimeshakubaliana kuhusu Uhamisho huu wa Kagawa na inasadikiwa Dili hii itagharimu Pauni Milioni 17.

Ikiwa Kagawa, mwenye Miaka 23, atafuzu upimaji afya yake itabidi asubiri kupatiwa Kibali cha Kufanya Kazi Nchini Uingereza ambacho huenda ikabidi Man United kukikatia Rufaa kwa vile Mchezaji huyo hajatimiza lile sharti la kuchezea Timu ya Taifa ya Japan Mechi zinazozidi Asilimia 75 ambazo Timu hiyo imecheza katika Miaka miwili iliyopita.
Akimzungumzia Kagawa, Kocha wa Timu ya Kwanza ya Man United, Rene Meulensteen, amemwagia sifa na kusema Mchezaji huyo amekamilika kama Kiungo Mshambuliaji.
Rene Meulensteen ametamka: ‘Ni mwepesi, anaeweza kucheza pasi moja au mbili, kufungua nafasi na kufunga mabao!’
Katika Misimu miwili aliyokuwa na Borussia Dortmund, Kagawa ametwaa Ubingwa wa Bundesliga mara mbili na German Cup mara moja na amechezea Klabu hiyo mara 71 na kufunga bao 29 na kusaidia bao 15.
Shinji Kagawa atakuwa Mchezaji wa 5 toka Japan kucheza kwenye Ligi Kuu England wengine wakiwa ni Junichi Inamoto (Arsenal na Fulham), Kazuyuki Toda (Tottenham), Hidetoshi Nakata (Bolton), na Ryo Miyaichi (Arsenal na Bolton).
Kwa Man United, Kagawa atakuwa ndie Mchezaji wa kwanza kutoka Japan na kuifanya Man United kuwa Klabu ya kwanza kuwa na Wachezaji kutoka Japan, South Korea na China.
No comments:
Post a Comment