Katika Mechi hiyo England iliifunga Ukraine bao 1-0 na kuwatupa Wenyeji hao wa Mashindano nje.
Kwa mara ya kwanza jana, Rais wa FIFA, Sepp Blatter, alijitokeza waziwazi na kuunga mkono Teknlojia ya kuamua kama Mpira umevuka mstari wa Goli, GLT [Goal Line Technology].
Blatter aliposti kwenye Mtandao wake wa Twitter: ‘GLT si kitu cha hiari, ni lazima!’
Bodi ya Kimataifa ya Vyama vya Soka, International Football Association Board, IFAB, iliyoketi huko England Mwezi Machi ilitamka kuwa uamuzi wa kuruhusu utumiaji wa teknolojia ya kisasa iliyo majaribioni katika kugundua kama mpira umevuka mstari wa goli au la, GLT, utafanyika kwenye Kikao kijacho cha Julai 5 huko Kiev, Ukraine mara baada ya kumalizika kwa EURO 2012.
Teknlojia hiyo ilikuwa majaribioni na Makampuni manane yalikuwa yakifanya majaribio lakini Kikao hicho kilizibakisha Kampuni mbili, Hawk-Eye na GoalRef, kuendelea majaribio yao kwa Miezi miwili zaidi.
IFAB inaundwa na Vyama vya Soka vya Visiwa vya Uingereza, yaani vile vya England, Wales, Scotland na Ireland, ambao ndio wanachukuliwa kama waanzilishi wa mchezo wa Soka, na Wawakilishi kutoka FIFA.
Mabadiliko yeyote ya Sheria za Soka lazima yapitie IFAB ambako hupitishwa ikiwa tu Kura 6 kati ya 8 zilizopo zitaunga mkono na mgawanyo wa Kura hizo 8 ni moja kwa kila Chama cha Soka cha England, Wales, Scotland na Ireland huku FIFA wakiwa na Kura 4.
Kawaida mabadiliko yeyote ya Sheria huanza kutumika kuanzia Julai Mosi kabla Msimu mpya wa Soka haujaanza.
No comments:
Post a Comment