Hata hivyo, IFAB, ambayo ndio pekee yenye mamlaka ya kubadili Sheria za Soka, imesisitiza kuwa Mifumo hiyo ni ya kusaidia Marefa na si ambayo itatoa maamuzi kwani Marefa watabakia ndio wenye uamuzi wa mwisho.

IFAHAMU IFAB
IFAB inaundwa na Vyama vya Soka vya Visiwa vya Uingereza, yaani vile vya England, Wales, Scotland na Ireland, ambao ndiyo wanachukuliwa kama waanzilishi wa mchezo wa Soka, na Wawakilishi kutoka FIFA.
Mabadiliko yeyote ya Sheria za Soka lazima yapitie IFAB ambako hupitishwa ikiwa tu Kura 6 kati ya 8 zilizopo zitaunga mkono.
Mgawanyo wa Kura hizo 8 ni moja kwa kila Chama cha Soka cha England, Wales, Scotland na Ireland huku FIFA wakiwa na Kura 4.
Majaribio hayo ya Hawk Eye na GoalRef yalisimamiwa na Wataalam kutoka Maabara ya Uswisi, EMPA [Swiss Federal Laboratory for Materials Science and Technology].
Hawk Eye inatumia Kamera na mfumo wa GoalRef unatumia mtandao wa sumaku na kila mfumo hupeleka haraka kwenye Saa inayovaliwa na Refa ikiwa mpira utavuka mstari wa Goli na hivyo kutakiwa kuhesabiwa kama Goli halali.
Ikiwa IFAB itapitisha matumizi ya Mifumo hiyo matumizi yake yatachukua muda kwa Vile Viwanja vya Soka vitabidi vifungwe mitambo hiyo lakini inategemewa Teknlojia hii huenda ikaanza kutumika rasmi kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa ya Dunia itakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.
No comments:
Post a Comment