BUKOBA SPORTS

Saturday, June 16, 2012

TWIGA STARS WATUNGULIWA NA ETHIOPIA GOLI 1-0, WATUPWA NJE FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA !


Mchezaji wa timu ya Twiga Stars Mawanahamisi Omary akiondoka na mpira kuelekea goli la timu ya wanawake ya Ethiopia huku mabeki wa timu hiyo wakiwania mpira huo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka ujao, mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Dar es salaam jioni hii.

Marefa wakiongoza timu za Ethiopia na Twiga Stars wakati zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo huo jioni hii.

Wachezaji wa timu za wanawake wa Tanzania na Ethiopia wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.

Wachezaji wa Twiga Stars na Ethiopia wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Mpira umekwisha ambapo Twiga Stars imefungwa goli moja kwa bila na timu ya wanawake ya Ethiopia na kuwasukumiza nje ya mashindano hayo , Timu ya wanawake ya Ethiopia ilikuwa ikifanya mashabulizi mengi na ya nguvu katika lango la Twiga Stars kwa muda mrefu na dalili zilionyesha kwamba wataweza kupata goli pamoja na kwamba walikuwa wakicheza ugenini

Timu ya Taifa ya wanawake, Twiga stars, Imepoteza tiketi ya kwenda kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake baada ya kufungwa bao 1-0 kutoka kwa Ethiopia.
Twiga stars imetolewa kwa jumla ya bao 3-1 baada ya hapo kabla Kufungwa bao 2-1 huko Ethiopia.

No comments:

Post a Comment