Poland imejiongezea matumaini ya kuvuka salama mechi za makundi.
Kwa sare hiyo, Poland ina matumaini kwamba huenda ikavuka mechi za makundi.
Poland, ambayo inashirikiana na Ukraine katika kuandaa mashindano ya Euro 2012, tayari ilikuwa imelemewa bao 1-0 kabla ya kufanikiwa kusawazisha, kupitia nahodha Jakub Blaszczykowski katika kipindi cha pili, na kwa mkwaju wa mguu wa kushoto.
Urusi walikuwa wamefanikiwa kuongoza walipopata bao katika dakika ya 37, kupitia mshambulizi hodari Alan Dzagoev baada ya kupigiwa pasi safi na Andrey Arshavin.
Timu zote zilionyesha mchezo wa hali ya juu, na kulikuwa na uwezekano wa kila timu kujipatia ushindi.
Matokeo hayo yanamaanisha ushindani ni wazi katika kundi A, na kimahesabu timu zote nne katika kundi hilo zinaweza kufuzu kuingia robo fainali.
MASHABIKI WA POLAND WAKISHANGILIA KWA WINGI!
HAPA MASHABIKI WA RUSSIA WAKIWEKA BANGO KUONYESHA MSISITIZO!
No comments:
Post a Comment