BUKOBA SPORTS

Wednesday, June 13, 2012

MANCHESTER UNITED YAMSAINI NICK POWELL TOKA CREWE ALEXANDRA

United he stands: Nick Powell has signed for Manchester United
Manchester United wamemsaini Kinda wa Miaka 18, Nick Powell, kutoka Timu ya Daraja la chini huko England, Ligi 1, Crewe Alexandra kwa dau ambalo halikutangazwa.
Powell, anaechezea Timu ya Taifa ya England ya Vijana chini ya Miaka 18, aliifungia Crewe bao 16 katika Mechi 45 alizocheza Msimu wa 2011/12.

                                                     NICK POWELL (KULIA)
NI NANI Nick Powell?
•Alizaliwa Crewe Machi 1994 na kujiunga na Klabu ya Crewe akiwa na Miaka 5 tu
•Alianza kuichezea Timu ya Kwanza ya Crewe akiwa na Miaka 16.
•Amechezea Timu za Taifa za Vijana za England za chini ya Miaka 16 na 17.

Akiongelea usajili huu, Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson said: "Ni kipaji pekee na amefundishwa vyema huko Crewe."
Nae Powell alizungumza: “Kusaini Manchester United ni ndoto iliyotimia!”

No comments:

Post a Comment