BUKOBA SPORTS

Saturday, July 14, 2012

LIVERPOOL WAKAMILISHA USAJILI WA BORINI

Fabio Borini atua Liverpool
Liverpool wametangaza ya kuwa Fabio Borini amejiunga na klabu hiyo baada ya kufanya vipimo vya afya na kisha kusaini mkataba na klabu hiyo.

Fabio Borini atua Liverpool..
Mchezaji huyo mwenye asili ya Italia amefanya vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wake huo mpya na Liverpool.
Kutua kwake Liverpool kumemfanya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Brendan Rodgers.
Borini na Rodgers wanafahamiana vizuri kwani wameshafanya kazi pamoja wakati wakiwa Chelsea, Swansea na sasa safari yao yaendelea wakiwa Liverpool.

Kwenye vipimo
Uwezo wa Borini wa kucheza na nyavu umeweza mfanya mpaka akachaguliwa katika kikosi cha taifa cha Italia amabacho kilishiriki katika mashindano ya Euro.
“Liverpool inafuraha kutangaza ya kuwa imemsajili mchezaji wa AS Roma Fabio Borini.
Mchezaji huyo wa Italia amesaini mkataba wa muda mrefu na klabu hii baada ya kufanikiwa kupita vipimo vya afya.
Kujiunga kwake na Liverpool kunamfanya awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Brendan Rodgers” ilisema taarifa toka kwenye website ya Liverpool.

Borini atavaa jezi namba 29 kwani ndo namba aliyoiomba apewe na kusema ya kuwa ndio namba ya bahati kwake.
“Nataka kufunga magoli na kuweza ifikisha Liverpool Champions League na kuisadia Liverpool kwa kila namna .
Sina kikubwa cha kusema ila, kupitia kwa Brendan Liverpool itacheza mpira tena mpira wa kuvutia“. Alisema Borini.

MAXI RODRIGUEZ AIHAMA LIVERPOOL
Maxi Rodriguez
Liverpool imetangaza ya kuwa mchezaji wao Maxi ameondoka klabuni hapo na kurudi nchini kwake Argentina kujiunga na klabu yake ya zamani ya Newell’s Old Boys.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitua Liverpool akitokea Atletico Madrid Januari 2010 na kuweza fanikiwa kufunga magoli 17 katika mechi 73 alizochezea timu ya Liverpool.
Kocha mpya wa Liverpool Rodgers alijaribu mshawishi mchezaji huyo kubakia lakini jitihada hizo zimegonga ukuta, baada ya Maxi kuamua kurudi katika klabu yake ya zamani alioacha miaka 10 iliyopita.

Website ya Liverpool imesema ya kuwa,
“Liverpool FC amethibitisha ya kuwa Maxi amejiunga na Newell’s Old Boys ya Argenrtina.
Kila mtu kutoka Liverpool FC kwapamoja twapenda tumshukuru Maxi kwa msaada wake alioutoa na twamtakia kila lililo la kheri mbeleni“.
Maxi nae aliwaandikia barua mashabiki wa Liverpool isemayo,
“Dear Reds, Mie Naondoka Liverpool FC leo.
Kabla sijajiunga na LFC, nlikuwa naijua ni klabu tu ambayo ni kubwa Ulimwenguni katika maswala ya mpira kama klabu nyinginezo. Lakini baada ya kuhamia hapa nimegundua kuwa hii sio klabu kubwa tuu ila ni Familia kubwa na nzuri.
Nimejaribu kucheza kwa uwezo wangu wote pindi nlipokuwa naivaa jezi ya Liverpool. Imekuwa ni faraja kwangu kuweza kuivaa na kuitetea jezi hii ya LFC kwa mda wote huu wa miaka miwili na nusu. Ninarudi nyumbani na sunduku ambalo limejaa kumbukumbu nyingi nzuri kuhusu hapa, marafiki wazuri nliowapata na pia Familia nzima ya LFC.
Nashukuru sana kwa msaada na ukarimu wenu. Ni vigumu kueleza ni kiasi gani faraja nliyokuwa naipata pindi The Kop walipoimba jina langu katika wimbo,… ‘Maxi, Maxi Rodriguez runs down the wing for me da da da dada…’
Hasta la vista“.
Maxi.

No comments:

Post a Comment