BUKOBA SPORTS

Friday, July 13, 2012

LIVERPOOL WAKUBALIANA NA ROMA UHAMISHO WA BORINI

Klabu ya soka ya Liverpool ya Uingereza imefikia makubaliano na klabu ya AS Roma ya Italia juu ya ada ya uhamisho wa mshambuliaji wa timu hiyo ya Italia Fabio Borini. Gazeti la the sun laUingereza linadai kuwa Borini ndiye atakua mchezaji wa kwanza kusainishwa na kocha wa majogoo hao wa jiji Brendan Rogers na inasemekana dili hilo litakamilika masaa 48 yajayo. Usajili huo utamuweka mshambuliaji wa klabu hiyo Andy Carroll katika wakati mgumu kuendelea kubaki klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment