BUKOBA SPORTS

Sunday, July 22, 2012

LIVERPOOL WATOSHANA NGUVU NA TORONTO KWA GOLI 1-1

morgan akifunga
Jana ndiyo ilikuwa mechi ya kwanza kwa Brendan Rodgers kuiongoza timu yake ya Liverpool na mechi hiyo iliisha kwa sare ya magoli,baada ya mshambuliaji wa akiba wa Liverpool Adam Morgan kuweza kufunga goli lake la kwanza kwa timu yake hiyo na hivyo kuweza kuifanya timu yake hiyo kutoka kiwanjani hapo na matokeo ya sare.My ball: Liverpool's Suso, left, skips past Toronto FC's Matt Stinson and Aaron Maund
Morgan jana aliweza msaidia Rodgers aanze maisha yake kama kocha wa Liverpool kwa amani kidogo baada ya kumuokoa na kipigo kutoka kwa timu ya Toronto.
Pacheco na Jose
Charle Adam
Skrtel (kulia) na jonjo
Timu hiyo ya Toronto ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Quincy Amarikwa lakini hazikupita dakika nyingi Liverpool walisawazisha kupitia kwa Adam Morgan baada ya Raheem Sterling(mwenye umri wa miaka 17) kufanya kazi kubwa ya kuwachambua mabeki na kisha kumsogezea Morgan (mwenye umri wa miaka 18) ambaye alitupia nyavuni mpira bila ya makosa.
Suso
raheem sterling
Lucas na Rodgers
Rodgers alichezesha timu mbili tofauti katika vipindi vyote vya mchezo wa jana. Katika kipindi cha kwanza alichezesha wachezaji 11 ambao katika kipindi cha pili wote walitoka na wakaingia wachezaji 11 wengine.
Rogers Centre
Liverpool (first half 4-3-3): Jones: Wisdom, Sama, Carragher, Enrique: Aquilani, Spearing, Adam: Ibe, Ecclestone, Pacheco.
Liverpool (second half 4-3-3): Gulacsi: Flanagan, Skrtel, Wilson, Robinson: Adorjan (Lucas 74mins), Shelvey, Suso: Cole, Morgan, Sterling.
Subs: Lucas, Smith, Ward, McLaughlin
Goal: Morgan (69)

No comments:

Post a Comment