Timu ya Tottenham imetangaza rasmi ya kuwa imefanikiwa kumsajili mchezaji Gylfi Sigurdsson kutokea Hoffenheim.
Sigurdsson mwenye umri wa miaka 22, alipata umaarufu pindi alipokuwa kwa mkopo Swansea akitokea Hoffenheim,akiwa chini ya kocha Brendan Rodgers.
Alitarajiwa angesaini mkatabawa kudumu na Swansea lakini baada ya Rodgers kuhamia Liverpool Sig ikasemekana atahamia Liverpool lakini mwishowe ametua timu ya Tottenham.
Taarifa toka katika website ya Tottenham inasema “Tunafuraha kutangaza ya kuwa tumekamilisha usajili wa mchezaji Gylfi Sigurdsson aliyekuwa akichezea Hoffenheim”
sigurdsson ambaye alifanikiwa kufunga magoli 7 katika mechi 19 alizocheza akiwa Swansea ndo amekuwa usajili wa kwanza wa Tottenham kuufanya tokea kutangazwa kwa kocha wao mpya AVB.
No comments:
Post a Comment