Wema na Wolper wakiwa katika pozi baada ya mpambano wao.
Na Hamida Hassan MASTAA wa filamu Bongo, Jackline Wolper na Wema Sepetu wamepongezwa na wadau kwa uamuzi waliochukua wa kumaliza bifu lao kwa kuchangia mfuko wa elimu Tanzania.
Wolper na Wema, mwishoni mwa wiki iliyopita walipanda ulingoni ndani ya Uwanja wa Taifa kupigana katika Tamasha la Matumaini ambapo sehemu ya fedha iliyopatikana ilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana nchini.
Wakizungumza na Ijumaa mara baada ya tamasha hilo, baadhi ya wadau wa filamu walisema walichokifanya mastaa hao ni kitu cha busara kwani wamechangia elimu lakini pia wametumia pambano hilo kumaliza tofauti zao.
No comments:
Post a Comment