Brendan Rodgers na Nuri Sahin
Liverpool wamefanikiwa kumsajili mchezaji wa Real Madrid Nuri Sahin kwa mkopo baada ya mchezaji huyo kushawishiwa na Xabi Alonso ili aweze kwenda Liverpool.
Sahin
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na kocha huyo wa Liverpool baada ya kutanguliwa na usajili wa Joe Allen, Fabio Borini na Oussama Assaidi.
Liverpool wameweza wapiku Arsenal katika usajili wa mchezaji huyo baada ya mchezaji huyo kudhihirisha ya kuwa alishauriwa na Alonso ili aweze tua Liverpool.
“Ndio, mara nyingi sana Xabi alinishawishi nije Liverpool, Xabi napenda sana mpira na anaipenda Liverpool.
Nlipofika Madrid tulikuwa twaongelea sana mpira wa Ujeruman na Italia. Sasa pindi aliposikia Liverpool yanitaka, akaanza kunihadithia kuhusu Liverpool.
Anamapenzi ya dhati na Liverpool Football Club, yaani utasema kama chizi alivyokuwa akiiongelea Liverpool. Kila mda alikuwa akiniambia NENDA KULE, UTAPAPENDA. Mashabiki watakupokea vizuri na kukupenda na mambo kama hayo.
Akasema Anfield ndio uwanja bora duniani. Xabi ameshinda makombe na Liverpool na nategemea na mie ntayapata.
Jose Mourinho nae alimshauri Sahin kuja Ligi ya Uingereza kwa kumwambia ya kuwa,
“Premier League ni ligi bora na nzuri kwa kila mchezaji.
Kila wikiendi utakuwa unafurahia mpira wako. Pia akasema ni kivipi ambavyo aliwahi fanya kazi na Brendan Rodgers pindi walipokuwa Chelsea, akasema Rodgers ni mtu safi na kocha bora sana.” Alisema Sahin
Sahin vipimoni
Rodgers nae hakusita kumshukuru Bosi wake wa zamani kwa kumletea mchezaji huyo,
“Jose ametusaidia kuweza kutuletea mchezaji mwenye kiwango kama cha Sahin.
Kwangu mchezaji akiwa na ufundi huwa inanipa raha sana. Nina wachezaji wazuri sana hapa lakini Sahin ni mzuri pia na tena anauzoefu.
Pindi tulipojua tu kuwa yupo sokoni tulijitahidi kwa kila namna aje kwetu na sio Arsenal.
Hatimaye amekuja na kwahilo twashukuru.” alisema Rodgers
FC TWENTE WAMSAJILI BOYATA WA MAN CITY
Dedryck Boyata FC Twente wamefanikiwa kumpata mchezaji wa Man City Dedryk Boyata kwa mkopo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ametua klabuni hapo na hivyo kupelekea uvumi wa kuwa mchezaji Douglas wa hapo FC Twente anaweza kwenda Uingereza huku klabu za Newcastle na Fulham zikiwa zamgombania na taarifa zaidi zadai ya kuwa Fulham tayari wameshatoa paundi mil 4 na huku Newcastle wakiwa wametoa paundi mil 4.5
CHELSEA WAMSAJILI TENA AZPILICUETA TOKA MARSEILLE.
Cesar Azpilicueta ataanza mazoezi na wachezaji wenzake wapya wa Chelsea baada ya kuweza kamilisha uhamisho wake toka Marseille ya Ufaransa.
Beki huyo wa kushoto wa Kihispania mwenye umri wa miaka 22 ametua klabuni hapo kwa ada ya paundi mil 7 huku akianguka saini ya miaka mitano na klabu hiyo ya Chelsea.
Beki wa chelsea Ashley Cole alisema pitia mtandao wa Twitter kuwa,
“Tumefanya mazoezi na beki wetu mpya wa kulia leo Cezar azpilicueta na natarajia kumuona Victor Moses akijiunga nasi karibuni, wachezaji wadogo wawili ambao ni wazuri sana.”
“Kama kuondoka kwangu kutawasaidia Marseille kifedha basi ni uhamisho ambao umewanufaisha kila pande.
Naishukuru klabu pamoja na mashabiki kwa mapenzi yao kwangu hata pale mambo yalipokuwa sio safi walitusapoti.” alisema Azpilicueta.
Mchezaji huyo mpya hatopata tabu katika nafasi yake ya beki wa kulia kwani Ivanovic ambaye amekuwa akicheza upande huo amekuwa akitaka kucheza katikati kila kukicha na sio kama beki wa pembeni.
No comments:
Post a Comment