Swansea wamekamilisha usajili wa paundi mil 5.5 wa mchezaji Ki Sung-Yeung toka Celtic.
Mchezaji huyo hatoweza cheza mechi ya Jumamosi kutokana na bado hajapata kibali cha kuchezea Uingereza.
Ki mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitatu na kusema,
“Pindi ninapoingalia Swansea naona klabu ambayo inakuwa na aina yake ya uchezaji inanivutia.
Mwaka jana nlikuwa nawaangalia sana na kiukweli walikuwa tofauti kabisa na klabu zingine. Walikuwa wanamiliki mpira na kupiga pasi kila dakika na kwangu hicho ni kitu nachokipenda. Nadhani kuja kwangu hapa kutanisaidia mie kukua kimpira na pia kutaisaidia klabu.”
Mwenyekiti wa Swansea nae akasema,
“Baada ya kumpoteza Joe Allen, ilikuwa ni muhimu kuzitumia hela vizuri na kuweza leta wachezaji wenye ubora ambao wataipeleka klabu mbele.
Ki inao huo ubora tunaoutafuta na kila mtu katika klabu amefurahishwa na ujio wake.
Uwezo wake wa kukaba na uharaka wake umekuwa ukionekana kwa kila mtu na kusema ukweli ataingia katika timu yetu bila matatioz”
No comments:
Post a Comment