Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kwamba sababu ya kumtimua kocha huyo ni kitendo cha kumpanga nyota wa timu hiyo Mrisho Ngassa katika mechi ya fainali ya Kombe la Kagame baina ya Azam na Yanga ambapo Yanga ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Azam mabao 2-0.
Inaelezwa kuwa uongozi ulikerwa na kitendo cha Ngassa ambaye kwa muda mrefu amekuwa akituhumiwa kuwa na ‘Uyanga’ na hivyo kocha kumuweka benchi katika mechi za kombe la Kagame, alipoibusu na kuvaa jezi ya Yanga baada ya mchezo baina ya Azam na Vita.
No comments:
Post a Comment