BUKOBA SPORTS

Wednesday, August 1, 2012

MRISHO NGASSA ATUA SIMBA KWA MIL.25!

Biashara na Mjadala wa Mrisho Ngasa umefungwa leo mchana saa tisa kasorobo baada ya Simba SC kuizidi nguvu Yanga na kutoa shilingi milioni 25. ofa ya Yanga iliiishia milioni 20.
Azam FC inamtakia kila la heri na mafanikio mema Mrisho Ngasa kwenye klabu yake mpya ya Simba
 Ngassa ameitumikia Azam FC kwa misimu miwili ambapo ameweza kuwapa taji la Kombe la Mapinduzi mwaka 2012, kuwezesha Azam FC kushika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2011/12 pamoja na Kagame Cup 2012 nafasi ya pili.
Ngassa amefanikiwa kuibika mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara katika msimu wake wa kwanza wa ligi kuu Tanzania kwa kuifungia Azam FC goli 16.  

 http://azamfans.blogspot.com

No comments:

Post a Comment