Maskini Arsenal ... wadau wasema kiwango chao bado!!
Kwa mara ya pili mfululizo, Arsenal wametoka sare ya 0-0 na safari hii ni Uwanjani Britannia na Stoke City katika Mechi ya Ligi Kuu England licha ya kuitawala Mechi yote, Aslimia 67 kwa 33, kupataKona 11 kwa 0, kupiga Shuti 17 kwa 6 lakini ni Mashuti mawili tu ndio yaliyolenga Golini na takwimu hizo zote zinalenga kuonyesha pengo kubwa aliloacha Nahodha wao Robin van Persie alietimkia Manchester United ambae Msimu uliopita aliwafungia Mabao 30 ya Ligi.Wiki iliyopita wakicheza kwao Uwanja wa Emirates, Arsenal walitoka sare 0-0 na Sunderland katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu.
Ni mapema mno kuwaponda Arsenal na kuwatupa nje ya kinyang’anyiro cha Ubingwa lakini inabidi wajinoe kuondoa ubutu wao wa kufunga Mabao ambayo wanastahili kwa jinsiwanavyotawala Mechi.
Mechi yao inayofuata ni Anfield na Liverpool Jumapili Septemba 2.
VIKOSI:
Arsenal: Mannone, Jenkinson, Vermaelen, Mertesacker, Gibbs, Podolski, Diaby, Arteta, Cazorla, Gervinho, Giroud
Akiba: Martinez, Santos, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Djourou, Coquelin
Stoke City: Begovic, Wilkinson, Huth, Shawcross, Wilson, Pennant, Cameron, Whelan, Kightly, Walters, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Upson, Delap, Shotton, Jerome.
Refa: Lee Mason
No comments:
Post a Comment