Serena Williams.
MCHEZA tenisi nyota wa Marekani Serena Williams anatarajiwa kukutana na Victoria Azarenka wa Belarus katika nusu fainali ya michuano ya Olimpiki baada ya mmarekani huyo kumfunga Caroline Wozniacki katika mchezo wa robo fainali. Williams ambaye ana medali mbili za dhahabu katika michuano hiyo alimfunga kirahisi Wozniacki kwa 6-0 6-3 wakati Azarenka ambaye anashika namba moja katika orodha za ubora kwa upande wa wanawake alimfunga Angelique Kerber kwa 6-4 7-5.
No comments:
Post a Comment