BUKOBA SPORTS

Friday, August 3, 2012

ARSENAL WAKAMILISHA USAJILI WA KIUNGO WA HISPANIA - SANTIAGO CAZORLA!

Hatimaye klabu ya Arsenal wamekamilisha usajili wa kiungo wa Hispania, Santiago Cazorla kutoka klabu ya Malaga, mchezaji huyo amesema kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter.

"Sasa naweza kusema mimi ni mchezaji mpya wa Arsenal," alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.



Cazorla, ambaye ameichezea timu yake ya taifa mara 47 lakini alikosa ubingwa wa Kombe la Dunia kutokana na kusumbuliwa na ngiri, aliiwezesha Malaga kufuzu kucheza Ligi ya Klabu Bingwa wakati klabu yake ya zamani ya Villarreal ilishuka daraja.
KWA HISANI YA SHAFIHDAUDA

No comments:

Post a Comment