BUKOBA SPORTS

Thursday, September 13, 2012

AGUERO AISHUSHA PUMZI MANCHESTER CITY!

Manchester City imeshusha pumzi kutokana na mchezaji mshambuliaji wao, Sergio Aguero kuanza kujifua baada ya kuwa na majeruhi wa goti kwa wiki kadhaa ambapo sasa jumanne atasafiri na timu yake kwenda kuivaa Real Madrid katika michuano ya ligi ya mabingwa.
Aguero, 24, hajacheza mechi yoyote ya ligi kuu England tangu acheze ile ya kwanza ya Southampton na kuumia katika dakika ya 14 baada ya kuvaana na beki Nathaniel Clyne.
Kocha wa City, Roberto Mancini alisema anatumaini Aguero atakuwa fiti, ingawa hana uhakika kama ataweza kucheza katika mechi ya Ligi kuu England dhidi ya Stoke Jumamosi.

No comments:

Post a Comment