BUKOBA SPORTS

Thursday, September 13, 2012

WENGER KUONGEZWA MKATABA ARSENAL.

Klabu ya Arsenal ya Uingereza inapanga kumuongeza mkataba meneja Arsene Wenger ili aendelee kuinoa klabu hiyo yenye maskani yake jijini Kaskazini mwa jiji la Landon. Mkataba wa sasa wa Wenger unatarajiwa kuisha mwaka 2014 na kumekuwa na tetesi kuwa kocha anaweza kustaafu kufuatia kushindwa kuipa timu hiyo mataji kwa kipindi cha miaka saba. Lakini Ofisa Mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis amekuwa akimkingia kifua Wenger mwenye umri wa miaka 62 na kusisitiza kuwa klabu hiyo imejipanga ili kumaliza ukame wa kukosa vikombe kwa miaka saba. Akihojiwa Gazidis amesema kuwa ukiacha suala la kukosa vikombe kwa kipindi kirefu lakini kocha huyo amekuwa akiongoza klabu hiyo vyema na kuwa mojawapo ya klabu kubwa barani Ulaya.
KUHUSU ARSENE WENGER

Arsène WengerArsène Wenger, OBE is the manager of English Premier League side Arsenal. He is the club's longest serving manager and most successful, winning 11 individual honours since 1996. 
Born: October 22, 1949 (age 62), Strasbourg
Height: 1.91 m
Spouse: Annie Brosterhous
Children: Léa Wenger
____________________________________________________

CAMERON AWAOMBA WAFIWA WA TUKIO LA HILLSBOROUHG. 
WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron amewaomba radhi watu waliopoteza ndugu zao na kueleza kama watu hao wamenyimwa haki mara mbili, kufuatia maafa yaliyotokea katika mji wa Hillsborough. Katika maafa hayo mashabiki wapatao 96 walikufa kufuatia taharuki uwanjani na kukanyagana tukio ambalo lilitokea katika Uwanja wa Sheffield mwaka 1989. Akizungumza baada ya kusoma ripoti huru ambayo ilifichua baadhi ya maelezo ambayo hayakuwa yamewekwa wazi hapo awali kufuatia mkasa huo, Cameron amesema maafisa wa polisi walishindwa kutekeleza wajibu wao kikamilifu, na kisha kuwalaumu mashabiki wa klabu ya Liverpool. Trevor Hicks, ambaye ni kati ya watu ambao wamekuwa wakiongoza kampeni ya kufahamu ukweli, alisema ripoti hiyo inaonyesha kwamba maisha ya wengi yangeliweza kuokolewa kama huduma za dharura zingepatikana kwa haraka mara tu baada ya mashabiki kuanza kukanyagana. Bwana Hicks, ambaye binti zake wawili walifariki katika mkasa huo, alisema sasa wao watashinikiza hatua za kisheria kufuatia makosa ya kihalifu zichukuliwe katika kuhakikisha waliohusika wataadhibiwa.
LiverpoolBwana Hicks, ambaye binti zake wawili walifariki katika mkasa huo, alisema sasa wao watashinikiza hatua za kisheria kufuatia makosa ya kihalifu zichukuliwe katika kuhakikisha waliohusika wataadhibiwa.
"Tunahisi tumepiga hatua mbele. Ukweli umepatikana leo, na haki inaanza kesho," alielezea.
Ripoti hiyo imetayarishwa na tume huru ya Hillsborough iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza chanzo cha maafa hayo, na ambayo ilipitia zaidi ya kurasa 450,000 za maelezo mbalimbali, katika kipindi cha miezi 18.
Familia za waliokufa kwa muda mrefu zilipinga maelezo ya awali kwamba wote ya waliofariki walikuwa tayari wamekata roho dakika 15 baada ya mechi kuanza saa tisa, au ubongo ulikuwa tayari umeshakufa.
Anne Williams anadai kwamba mwanawe Kevin bado alikuwa hai saa kumi siku ya mkasa, na ameitaka serikali kuanzisha uchunguzi mpya kuhusiana na kifo chake.
Jopo hilo ambalo liliendesha uchunguzi lilielezea kwamba kati ya watu 28 ya wale 96 waliokufa, sio kweli kwamba walikuwa na damu iliyoganda na kutoweza kuenea mwilini, na kuna ushahidi ambao unaonyesha kwamba watu 31 walikuwa na mioyo na mapafu ambayo bado yalikuwa yanafanya kazi hata baada ya mkanyagano.
Mshauri wa masuala ya matibabu katika jopo hilo, Dk Bill Kirkup, alieleza kwamba watu 41 kati ya 96 waliokufa wangeliweza kuokolewa kama wangelipata matibabu kwa haraka.

_______________________________________

No comments:

Post a Comment