Hata hivyo, Paul Lambert amesema:
“Kulikuwa hamna kitu. Kama kasema maneno yeyote mie sijali. Namuheshimu
kama Kocha na Mchezaji wa zamani. ”
Mancini alimpandishia Lambert mara baada ya Mchezaji wa Villa Joe Bennett kumparamia Kiungo wa Man City Gareth Barry.
Mancini ameeleza: “Nilimuuliza Refa wa
Akiba kama ipo Kadi ya Njano bila kuonyesha ishara kwa mikono kuonyesha
Kadi na yeye Lambert akanifuata mimi. Sikuwa naongea nae sasa kwa nini
anifuate.”
Aliongeza: “Nimechoshwa na hizi tabia
zao. Wengine wakienda Viwanja vikubwa hawasemi kitu. Mbona wakiwa Old
Trafford hawasemi kitu?”
MIGONGANO YA MANCINI na Mameneja wenzake:
=Sir Alex Ferguson - April 2012: Walivaana na ilibidi watenganishwe kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Etihad.
=Mark Hughes - Feb 2011:
Mabishano yalizuka kuhusu kupeana mkono mwisho wa Mechi na Mark Hughes
Meneja wa Fulham alietimuliwa Man City na nafasi yake kuchukuliwa na
Mancini.
=David Moyes - March 2010:
Mancini alipigwa Faini £20,000 na FA baada ya kupatikana na hatia ya
kumsukuma Meneja wa Everton David Moyes wakati wa Mechi akidai
anachelewesha mpira wakati alipoudaka mpira uliotolewa nje.
Katika Mechi hiyo ya jana na Aston
Villa, Man City mara mbili waliongoza kwa Mabao ya Mario Balotelli na
Aleksandar Kolarov alakini Villa wakasawazisha kwa Bao la kujifunga
mwenyewe Barry na jingine la Gabriel Agbonlahor.
Kisha Charles N'Zogbia na Agbonlahor
wakapiga Bao mbili katika Dakika 30 za nyongeza na kuwatupa nje ya
CAPITAL ONE CUP na pia kuwafanya Mabingwa hao wa England wawe
hawajashinda katika Mechi zao 4 hadi sasa.
No comments:
Post a Comment