BUKOBA SPORTS

Tuesday, September 11, 2012

LIGI KUU ZANZIBAR: MTENDE RANGERS 3 ZIMAMOTO 0

Na Ally Mohammed, COCONUT FM 88.2, Zenji
Katika muendelezo wa Ligi Kuu Zanzibar jana kulikuwa na Mechi moja iliyochezwa katika uwanja wa Amaan, mjini Unguja kwa kuwakutanisha Mtende Rangers, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu ikicheza na Kikosi cha Zimamoto.
Katika mechi hiyo iliyohudhuriwa na Watazamaji wachache ilimalizika kwa Mtende Rangers kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0 kwa mabao ya dakika ya ya 5 kupitia Ali Salum, bao la pili likifungwa na Ali Manzi katika dakika ya 42 huku msumari wa mwisho ukishindiliwa na Islah Khamis katika dakika ya 77.
Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi moja na ya mwisho katika mzunguko wa kwanza mechi itakayochezwa katika uwanja wa Amaan, majira ya saa 10:30 jioni kwa kuzikutanisha timu za Chuoni na Mundu.
LIGI KUU ZANZIBAR
[Zanzibar Grand Malt Premier League]
RATIBA/MATOKEO
Jumatatu Septemba 10
Mtende v Zimamoto [Amaan, Unguja]
Jumanne Septemba 11
Chuoni v Mundu [Amaan, Unguja]
Jumamosi Septemba 15
KMKM v Malindi [Amaan, Unguja]
Super Falcon v Duma [Gombani, Pemba]
Jumapili Septemba 16
Mafunzo v Bandari
Chipukizi v Jamhuri [Gombani, Pemba]
Jumatatu Septemba 17
Mtende v Chuoni [Amaan, Unguja]
Jumanne Septemba 18
Zimamoto v Mundu [Amaan, Unguja]
Jumamosi Septemba 22
KMKM v Bandari [Amaan, Unguja]
Super Falcon v Jamhuri [Gombani, Pemba]
Jumapili Septemba 23
Mafunzo v Malindi [Amaan, Unguja]
Chipukizi v Duma [Gombani, Pemba]
Jumatatu Septemba 24
Mtende v Mundu [Amaan, Unguja]
Jumanne Septemba 25
Zimamoto v Chuoni [Amaan, Unguja]

TIMU 12 ZINAZOSHIRIKI:
TOKA UNGUJA:
-Bandari
-Chuoni
-KMKM
-Mafunzo
-Malindi
-Mundu
-Mtende
Zimamoto
TOKA PEMBA
-Chipukizi
-Duma
-Jamhuri
-Super Falcon

No comments:

Post a Comment