BUKOBA SPORTS

Wednesday, September 5, 2012

TANZANIA YAPOROMOKA TENA VIWANGO FIFA.

 TANZANIA imeporomoka tena kwa nafasi nne katika viwango vya soka duniani vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutoka nafasi ya 128 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 132. Mabingwa mara tano wa Kombe Dunia bado wamendelea kusota nje ya kumi bora baada ya kupanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 13 mwezi uliopita mpaka nafasi ya 12 baada ya kushinda mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Sweden. Katika orodha hizo mabingwa wa Ulaya na Dunia, Hispani bado wameendelea kuwa vinara katika orodha hiyo wakifuatiwa na Ujerumani waliopo katika nafasi ya pili huku Uingereza nao wakibakia katika nafasi yao ya tatu waliokuwepo msimu uliopita. Ureno imekwea nafasi moja kutoka nafasi ya tano waliyokuwepo mwwezi uliopita mpaka nafasi ya nne wakiwateremsha Uruguay mpaka nafasi ya tano wakati nchi za Italia inayoshika nafasi ya sita, Argentina saba, Uholanzi nane, Croatia tisa na Denmark 10 zikikamilisha kumi bora ya orodha hiyo kwa kubakia katika nafasi zao ambazo walikuwepo msimu uliopita. Kwa upande wa tano bora za Afrika Ivory Coast bado inaendelea kuongoza kwa kuwepo katika nafasi ya 16 wakifuatiwa na Algeria ambao wamepanda kwa nafasi sita mpaka nafasi ya 28 huku Ghana wakishika nafasi ya tatu kwa kupanda nafasi moja mpaka nafasi ya 32. Tano bora kwa Afrika inakamilishwa na nchi za mali ambao wamekwea kwa nafasi saba mpaka nafasi ya 32 na Libya ni watano wakiwa wamepanda nafasi mbili mpaka nafasi ya 36 waliyofikia mwezi huu.

No comments:

Post a Comment