
Filamu Mpya Ya My Man Sehemu ya 2 inatarajiwa kuingia Sokoni muda si mrefu baada ya kumalizika na kukamilika kwa utayarishaji wa filami hiyo.
Filamu hiyo ya kitanzania ambayo story yake imeandikwa na Kijana Geric Kimaro anayesomea Shahada ya Kwanza ya Filamu katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akiwa mwanafunzi wa Mwaka wa 2 wa Chuo hicho.
Katika filamu hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya BORNAGAIN kwa kumshirikisha Nguli wa filamu za Bongo Mwenye Swaga za Uchungaji, Pastor Myamba." Mbali na Kumshirikisha Pastor Myamba filamu hiyo imewashirikisha wasanii wapya na kuna sura mpya nyingi ambazo ni vipaji na zao kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM).
Wengi wa washiriki wa filamu hiyo ni wanafunzi wanaosomea Shahada ya Kwanza ya Filamu, ambapo pia amefanya hivi kuonyesha na Kutambulisha vipaji ambavyo bado vipo Shuleni.
No comments:
Post a Comment