Mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester City, MARIO BALOTELLI amezua tafrani nyingine baada kupitiliza mpaka katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati alipotolewa katika dakika ya 55 na ROBERTO MANCINI katika mchezo baina ya timu hiyo na Sunderland uliochezwa jana. Masaa machache baada ya mchezo huo kumalizika ambapo City ilifanikiwa kushinda kwa mabao 3-0, BALOTELLI mwenye umri wa miaka 22 alionekana Uwanja wa ndege jijini Manchester akiondoka kuelekea kwao Italia. Kutokana na tukio hilo utaongeza msukumo kwa MANCINI kujaribu kumuuza mchezaji huyo mtukutu katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Katika mchezo huo BALOTELLI alionekana kutokuwa na furaha kwa jinsi mabeki wa Sunderland walivyokuwa wakimchezea katika kipindi chote ambacho alikuwa akicheza ndio maana MANCINI aliamua kumbadilisha na nafasi yake kuchukuliwa na SERGIO AGUERO kitendo ambacho nacho kilionekana kumuudhi. City haitafurahishwa na kitendo alichofanya mchezaji huyo cha kushindwa kwenda kukaa katika benchi la wachezaji wa akiba mpaka mpira utakapomalizika ingawa kuna uwezekano mdogo wa kupewa adhabu.
_________________________________________________________
FA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UBAGUZI DHIDI YA WACHEZAJI WA BOLTON.
Chama cha Soka nchini Uingereza-FA kinachunguza tuhuma za ubaguzi wa rangi zilizotolewa na mchezaji wa Bolton Wanderers MARVIN SORDELL wakati timu hiyo ilipofungwa na timu ya Millwall. SORDELL mwenye umri wa miaka 21 aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kuwa mbali nay eye kushambuliwa kwa maneno ya kibaguzi lakini pia yaliwalenga wachezaji wenzake LEE CHUNG-YONG, DARREN PRATLEY na BENIK AFOBE. Klabu hizo mbili pia zinachunguza tuhuma hizo zilizotolewa na Sordell ambaye anadai alisikia maneno hayo wakati anapasha misuli ili aweze kuingia katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Kwanza uliofanyika katika Uwanja wa The Den Jana. Msemaji wa Bolton amesema kuwa klabu hiyo kwa kushirikiana na Millwall watalifanyia uchunguzi tukio hilo kwa pamoja na wanatarajia kuzungumza maaskari waliokuwepo uwanjani pamoja na waamuzi wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment