BUKOBA SPORTS

Friday, November 9, 2012

AZAM YAWASIMAMISHA WACHEZAJI WAKE WATATU;SAID MORAD, ERASTO NYONI NA DEO MUSHI KWA TUHUMA ZA RUSHWA


BODI ya klabu ya soka AZAM FC imewasimamisha wachezaji wake WATATU , SAID MORAD ,ERASTO NYONI na DEO MUSHI kwa tuhuma za kupokea rushwa katika mchezo wake dhidi ya SIMBA uliomalizika kwa AZAM FC kufungwa magoli MATATU kwa MOJA.
Ofisa habari wa AZAM FC, JAFARI IDD, amesema wachezaji hao wamesimamishwa lengo likiwa ni kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.


Klabu hiyo itapeleka taarifa zake kwa chombo maalumu cha dola nchini kuchunguza tuhuma hizo.

No comments:

Post a Comment