BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 14, 2012

CHELSEA, FA WATUHUMIWA KULIFUNIKA SUALA LA CLATTENBURG.

KLABU ya Chelsea na Chama cha Soka nchini Uingereza-FA wametuhumiwa kufunika tuhuma zinazomkabili mwamuzi Mark Clattenburg kwa polisi. Polisi nchini humo walisitisha uchunguzi kuhusu Clattenburg kutumia lugha isiyokubalika kwa wachezaji wawili wa Chelsea ambapo tuhuma hizo zilifikishwa polisi na Jumuia ya Mawakili Weusi. Mwenyekiti wa jumuia hiyo Peter Herbert amesema kuwa suala hilo linaonekana wazi kwamba linataka linataka kufunikwa kimya kimya bila kulipatia ufumbuzi. Chelsea walifikisha malalamiko yao dhidi ya Clattenburg Octoba 29 kufuatia timu hiyo kufungwa na Manchester United mabao 3-2 siku moja baadae FA ilifungua uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo za Clattenburg kutumia lugha ya kibaguzi dhidi ya wachezaji hao kwenye mchezo huo. Polisi nao walianza uchunguzi kuhusiana na tukio hilo baada ya kupata malalamiko kwa maandishi kutoka kwa jumuia hiyo lakini polisi wameamua kulitupilia mbali suala hili kwa kuwa hakuna madai kuhusu tuhuma hizo kwasababu hakuna mhanga yoyote wa tukio hilo aliyejitokeza. FA wamethibitisha kuwa wataendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo lakini Herbert amechukizwa kwa kitendo cha FA au Chelsea kushindwa kufikisha suala hilo polisi.
______________________________________



MWANASOKA WA ZAMANI PELE ALAZWA.

Msemaji wa kituo cha afya cha Albert Einstein amesema kuwa mchezaji nguli wa zamani wa soka Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amelazwa katika kituo hicho kilichopo jijini Sao Paulo. Msemaji huyo alithibitisha hayo lakini alikataa kuelezea kwa undani zaidi kinachomsumbua nyota huyo mwenye umriwa miaka 72 ikiwa ni shinikizo kutoka kwa familia yake ambao hawakutana ugonjwa unaomsumbua nyota huo kuwekwa wazi. Kwa mujibu wa gazeti moja la michezo la Folha de Sao Paulo nyota huyo ambaye pia anajulikana kwa jina la utani la The King au Mfalme aliripotiwa kufanyiwa upasuaji wa nyonga. Pele anahesabiwa kama mmoja wapo ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika mchezo wa soka akiwa ameshinda Kombe la Dunia katika vipindi vitatu tofauti mwaka 1958, 1962 na 1970 huku akiwa amefunga mabao 1,281 katika kipindi chote alichosakata kabumbu.

No comments:

Post a Comment