BUKOBA SPORTS

Friday, November 30, 2012

FERGUSON AITOA CHELSEA MBIO ZA UBINGWA WA ENGLAND


sir Alex Ferguson
MANCHESTER, England
“Matokeo ya leo usiku yanatuweka sisi mbali kidogo na Chelsea katika mbio za ubingwa wa ligi. Sisi bado tuko mbele tukiongoza msimamo wa ligi, lakini Man City wako karibu yetu na msimu bado ni mrefu”
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekenulia meno mwanzo mbaya wa kocha wa Chelsea, Rafa Benitez klabuni Stamford Bridge, na kutabiri ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni kinyang’anyiro cha timu za jiji la Manchester.

Chelsea inayoshikilia ubingwa wa soka barani Ulaya, iko nyuma kwa pointi saba nyuma ya vinara Man United na sita, nyuma ya mabingwa watetezi Man City.

Fergie bosi wa Man United, alisema: “Matokeo ya leo usiku yanatuweka sisi mbali kidogo na Chelsea katika mbio za ubingwa wa ligi.

“Sisi bado tuko mbele tukiongoza msimamo wa ligi, lakini Man City wako karibu yetu na msimu bado ni mrefu.
“Umuhimu wa kushinda bao 1-0 katika baadhi ya mechi, unawaonesha wapinzani wako kiasi cha ujasiri mlichonacho.

“Kama utaangalia baadhi ya mechi muhimu za matokeo ya bao 1-0 tuliowahi kupata... rejea nyuma kabisa tulipoicaha Newcastle wakati wakiwa pointi tisa juu yetu mwaka 1996 – ushindi wetu wa 1-0 usiku huo, ukatuwezesha kutupa ubingwa.

“Kulikuwa na umuhimu wa ushindi wa 1-0. tulifanya hivyo kwa wengi wao.”

No comments:

Post a Comment