TAARIFA KAMILI TOKA TFF:
Release No. 177
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 3, 2012
MABADILIKO YA MECHI ZA VPL NAMBA 67,75,79,81 NA 82
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limefanya mabadiliko ya mechi hizo baada ya kutokea dharura, hivyo
kushindwa kufanyika kwa mujibu wa kanuni.
Sababu za mabadiliko hayo ni timu ya
Tanzania Prisons kupata ajali wakati ikienda Tanga kwa ajili ya mechi
dhidi ya Mgambo Shooting. Pia mvua kubwa iliyonyesha jijini Mwanza
ilisababisha kutofanyika kwa mechi ya Oktoba 31 mwaka huu kati ya Toto
Africans na Kagera Sugar.
Mechi hizo sasa zitafanyika kama
ifuatavyo; Mgambo Shooting vs Tanzania Prisons (14/11/2012- Mkwakwani,
Tanga), Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons (18/11/2012- Mabatini, Pwani),
Mtibwa Sugar vs JKT Ruvu (7/11/2012- Manungu, Morogoro), Kagera Sugar
vs Tanzania Prisons (4/11/2012- Kaitaba, Bukoba), na Ruvu Shooting vs
Toto Africans (4/11/2012- Mabatini, Pwani).
MABADILIKO MADOGO LIGI DARAJA LA KWANZA
Mechi mbili za Ligi Daraja la Kwanza
zimefanyiwa mabadiliko. Mechi kati ya Tessema vs Ndanda iliyokuwa
ichezwe tarehe 4/11/2012 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani sasa
itafanyika tarehe 5/11/2012 katika uwanja huo huo. Mabadiliko hayo
yanapisha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting vs Toto
Africans ambayo itachezwa 4/11/2012 kwenye uwanja huo huo.
Ashanti United vs Tessema zilizokuwa
zicheze Uwanja wa Mabatini 7/11/2012 sasa zitacheza siku inayofuata
(8/11/2012). Mabadiliko hayo ni kutoa fursa ya kupumzika kwa Tessema
ambayo 5/11/2012 itacheza na Ndanda.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment