SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limemfungia mechi mbili za Ulaya kocha msaidizi wa Manchester City, David Platt baada ya kutolewa na kupelekwa jukwaani wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid wiki iliyopita. Platt hataruhusiwa kuwepo katika benchi la wachezaji wa akiba wakati wa mchezo wa mwisho wa City dhidi ya Borussia Dortmund wiki ijayo. Katika taaifa ya UEFA`ambayo ilitumwa katika wavuti wake imesema kuwa Kamati ya Nidhamu ilimkuta na kosa Platt kwakuonyesha tabia isiyofaa katika mchezo huo hivyo kupelekea mwamuzi kumwamuru kwenda kukaa jukwaani. UEFA pia imeitoza faini ya paundi 12,000 klabu ya Manchester City baada ya wachezaji wake watano kupewa kadi za katika mchezo huo ambapo wamepewa siku tatu kama wanataka kukata rufani kuhusiana na adhabu hizo.
______________________________
Wahu Kupamba Uzinduzi Wa Dhana Ya “WELLNESS” Jumapili Hii Ubungo Plaza
Ila
afya hii inaweza kuwa ya kimwili (physical), kiakili (mental), kipesa
(financial), kinahusiano (relationship), kijamii (social),
kikazi(occupational), kiroho (spiritual), kihisia (emotional),
kimazingira (environmental) na hata ya kitabibu (medical).
Tunahitaji afya zote hizi kuwa kamili na wenye furaha (for optimal well-being).
Dhana hii ya WELLNESS
itaelezewa kwa ufupi kwa nini ni muhimu kwako katika hotel wa Blue
Pearl, Ubungo Plaza, jumapili tarehe 2 Desemba 2012 toka saa 8 mchana
hadi 1 jioni. Wataalam wenye uzoefu katika fani hii watakuelimisha kwa
muda mchache.
Uzinduzi huu utasindikizwa na mwanamuziki WAHU KAGWI toka Kenya akikuambia BETTER DAY. “Whatever you are going through today, there always gonna be a better day”.
Kiingilio: 20,000/= only per head
COME ONE, COME ALL.
Tickets
zitapatikana 8020 fashions Sinza, maduka yote ya Mariedo ambayo ni IPS,
Benjamini Mkapa Towers na Namanga , mlimani city Shear Illusions na
Milepamba shop Mwenge Bus stop.
NB: HAKUNA TIKETI ZITAKAZOUZWA MLANGONI SIKU YA JUMAPILI. Deadline Jumamosi saa 4 asubuhi. Only limited seats
NB: Get ready to step on GREEN CARPET for pictures, the carpet of HEALTH
No comments:
Post a Comment