BUKOBA SPORTS

Saturday, November 10, 2012

RATIBA YA MICHEZO YA ENGLISH PREMIER LEAGUE WIKIENDI HII: BIG MATCH - JUMAPILI MAN CITY vs SPURS, CHELSEA vs LIVERPOOL. LEO ASTON VILLA vs MANCHESTER UNITED, ARSENAL vs FULLHAM!

>>VINARA Man United wapo ugenini Villa Park!!
Timu zote 20 za Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League], zipo dimbani Jumamosi na Jumapili na vinara Manchester United Jumamosi Usiku wapo ugenini huko Villa Park kucheza na Timu inayosuasua Aston Villa, ambayo mara ya mwisho kuifunga Man United Uwanjani Villa Park ni Mwaka 1995, huku wakiwa na nafasi kubwa ya kulikuza pengo lao na Timu za nyuma yake  Chelsea na Man City kuwa kubwa lakini mvuto mkubwa upo kwa Mechi za Jumapili ambapo Chelsea wataikaribisha Liverpool na Man City kuwa wenyeji wa Tottenham Hotspur.

RATIBA:
Jumamosi, Novemba 10
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Fulham
Everton v Sunderland
Reading v Norwich City
Southampton v Swansea City
Stoke City v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v West Bromwich Albion
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Manchester United

Jumapili, Novemba 11
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool

ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI ZA MECHI za Jumamosi:
Arsenal v Fulham
Arsenal watamkosa Kiungo wao Jack Wilshere ambae yuko kwenye kifungo cha Mechi moja baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu walipofungwa 2-1 na Man United Wiki iliyopita.
Pia, Arsenal watawakosa Kipa Wojciech Szczesny, Aaron Ramsey na Alex Oxlade-Chamberlain ambao walikuwa majeruhi lakini wamepona ila bado hawajakuwa tayari kwa Mechi hii.
Fulham huenda wakamkosa Mahamadou Diarra ambae amekuwa akiuguza goti lake na Kocha wa Fulham, Martin Jol, amesema Mchezaji huyo yuko ‘fifte fifte’ kucheza.
Wakati huu, Arsenal wanahitaji ushindi ili kujipa matumaini baada ya kuanza vibaya kupita Msimu wowote ule wa enzi hizi za Ligi Kuu kwani, baada ya Mechi 10, wana Pointi 15 tu na wapo nafasi ya 7.
Rekodi ya Arsenal wakiwa Uwanja wa nyumbani kwa Fulham ni Ushindi Mechi 22 na Sare 4.


Aston Villa v Manchester United
Katika Mechi 31 walizocheza mwisho, Aston Villa wameifunga Man United mara moja tu na wataingia kwenye Mechi hii bila majeruhi Joe Bennet na Darren Bent na pia watamkosa Karim El Ahmadi ambae yupo kifungoni baada ya kujilundikia Kadi za Njano 5 na hivyo hatacheza Mechi moja.
Man United majeruhi wao ni Nani, Shinji Kagawa, Phil Jones na Nemanja Vidic na pia upo wasiwasi kama Jonny Evans atacheza baada ya kuumia kwenye Mechi ya juzi na Braga.

Everton v Sunderland
Everton watawakosa majeruhi Tony Hibbert, Darron Gibson na Victor Anichebe wakati Sunderland watamkosa James McFadden.

Southampton v Swansea
Wakati Southampton hawana majeruhi na hata Kipa wao Artur Boruc anatarajiwa kucheza baada ya kusafishwa kwa tuhuma za kumrushia shabiki wao chupa, Swansea watamkosa Chico Flores alieumia.

Stoke City v QPR
Stoke hawatakuwa na Rory Delap, Michael Owen na Marc Wilson ambao ni majeruhi na QPR watakuwa bila ya majeruhi Fabio na Andrew Johnson lakini pia Stephane M'Bia atakuwa nje akitumikia kifungo.

Reading v Norwich City
Hii ni Mechi muhimu mno kwa Reading ambao hawajashinda hata Mechi moja ya Ligi Msimu huu na wapo nafasi ya 18 wakiwa na Pointi 5 kwa Mechi 9.
Kwa Norwch, hali kidogo ni afadhali na wapo nafasi ya 14 wakiwa na Pointi 10  kwa Mechi 10.

Wigan AthleticWest Bromwich Albion
Wigan huenda wakamkosa majeruhi James McArthur ambae hajapona sawasawa lakini pia uhakika ni kuwa watawakosa Ryo Miyaichi na Albert Crusat ambao bado wanauguza maumivu yao.
West Brom watamkosa Kipa Ben Foster ambae ana matatizo ya nyonga.

MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 10 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Pointi 24
2 Chelsea 23
3 Man City  22
4 Everton 17 [Tofauti ya Magoli 6]
5 West Brom 17 [Tofauti ya Magoli 4]
6 Tottenham 17 [Tofauti ya Magoli 3]
7 Arsenal 15 [Tofauti ya Magoli 7]
8 Fulham 15 [Tofauti ya Magoli 5]
9 West Ham 15
10 Newcastle 14
11 Swansea 12
12 Liverpool 11 [Tofauti ya Magoli -2]
13 Wigan 11 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Norwich 10
15 Stoke 9
16 Sunderland Mechi 9 Pointi 9
17 Aston Villa 9
18 Reading  Mechi 9 Pointi 5
19 QPR 4
20 Southampton 4

WAFUNGAJI BORA:
TOP_SCORERS09NOV

No comments:

Post a Comment