BUKOBA SPORTS

Saturday, November 10, 2012

VODACOM PREMIER LEAGUE: TOTO AFRICA WAIFUNGA SIMBA GOLI 1-0 , AZAM 1 vs MGAMBO JKT 2, KAGERA SUGAR 0 vs POLISI MORO 0!!


Katika mchezo uliochezwa leo Uwanja Wa Taifa jiji Dar es salaam dhidi ya Simba na Toto Africa,Bao pekee la Mussa Said Kimbu dakika ya 73, leo limeizamisha Simba SC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Wachezaji wa Toto wakiwa wamebeba kocha wao Athumani Bilal kwa furaha ya ushindi leo

Kimbu alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Mganda, Mohamed Jingo tena akipitisha mpira katikati ya msitu wa mabeki wa Simba na kipa wao, Wilbert Mweta.


Katika michezo mingine ya ligi hiyo, Azam imefungwa 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwa matokeo hayo, Yanga inazidi kujinafasi kileleni kwa pointi zake 26, baada ya kucheza mechi 12 na kesho itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.



Wachezaji wa Toto wakinywa maji

Hatari kwenye lango la Toto

Komabil Keita wa Simba akionyesha ubabe na Suleiman Kibuta wa Toto. walitaka kupigana

RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Novemba 10
Mgambo JKT 2 Azam 1
African Lyon v Mtibwa Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
Simba 0 Toto Africans 1
Tanzania Prisons v JKT Ruvu [Sokoine, Mbeya]
Kagera Sugar 0 v Polisi Morogoro 0 [Kaitaba, Kagera]
JKT Oljoro v Ruvu Shootings [Sheikh Amri Abeid, Arusha]

Kesho Jumapili Novemba 11
Coastal Union v Yanga [Mkwakwani, Tanga]
 

No comments:

Post a Comment