BUKOBA SPORTS

Wednesday, November 7, 2012

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: SCHALKE 2 vs ARSENAL 2, REAL MADRID 2 vs BORUSSIA DORTMUND 2, MANCHESTER CITY 2 vs AJAX 2 - MALAGA, PORTO ZAFUZU!, CITY HOI..!!!

UEFA CHAMPIONS LIGI jana iliendelea na kuziona Timu mbili, Malaga na Porto, zote zikipata sare na zote kufuzu lakini kwa Klabu za England, hasa Mabingwa wao Manchester City, kufuzu kwao kunahitaji miujiza mikubwa baada ya kujitutumua na kutoka sare 2-2 na Ajax huku Arsenal nao wakitoka sare na Schalke lakini wao kufuzu kwao bado kuko mikononi kwao ingawa wanatishiwa na Olympiacos ya Ugiriki.

SCHALKE 1 vs ARSENAL 2 Arsenal wakiwa ugenini kucheza na Timu ya Ujerumani, FC Schalke, ambayo katika Mechi iliyopita huko Emirates, iliichapa Arsenal 2-0, LEO hii kipindi cha kwanza wameweza kupata magoli 2 dhidi ya Schalke, Goli la kwanza kwa Arsenal limefungwa na Theo Walcott dakika ya 18 na goli la pili likafungwa na Olivier Giroud dakika 26. Schalke wamejipatia Goli 1 ambalo limefungwa na mchezaji wao matata Klaas-Jan Huntelaar dakika 45 kipindi cha kwanza kabla ya kuisha.
Just getting started: Theo Walcott celebrates scoring the opening goal for Arsenal
Theo Walcott akishangilia baada ya kuipatia Timu yake goli la kwanza.
Giloud akishangilia goli la 2 Klaas Huntelaar akishangilia baada ya kuifungia goli la kwanza Schalke 04
Yellow peril: Walcott is mobbed after opening the scoring in Germany
Walcott akipongezwa nawenzake hapa
Level pegging: Schalke egualise with 67 minutes gone
Schalke04 dakika ya 67 wakisawazisha.

MATOKEO:
Jumanne Novemba 6
FC Dynamo Kyiv 0 FC Porto 0
Paris SaintvGermain FC 4 GNK Dinamo 0
FC Schalke 2 Arsenal 2
Olympiacos FC 3 Montpellier Hérault 1
RSC Anderlecht 1 FC Zenit St. Petersburg 0
AC Milan 1 Málaga 1
Manchester City 2 AFC Ajax 2
Real Madrid 2 Borussia Dortmund 2
MANCHESTER CITY vs AJAXWachezaji wa Ajax wakipasha kabla ya mchezo kuanza.
Huko England, ndani ya Etihad, Mabingwa wa England, Manchester City, walitoka sare ya 2-2 na Ajax Amsterdam katika Mechi ambayo Ajax waliongoza 2-0 ndani ya Dakika 17 za kwanza kwa bao za Nahodha wao Siem De Jong na Man City kusawazisha kwa bao za Yaya Toure, Dakika ya 22, na Sergio Aguero, Dakika ya 74.
Uso kwa uso tena meneja Roberto Mancini (kulia) akisalimiana na bosi wa Ajax  Frank De Boer kabla ya game kuanza.  Joe Hart
kipa wa City akiduwaa baada ya kufungwa.Roberto Mancini (kulia) akimwingiza Balotelli kwa ajili ya kuipatia ushindi Man CityHartbreak: City keeper Joe Hart is powerless to prevent Siem De Jong's opener, leaving Gael Clichy and Pablo Zabaleta aghast (below)
linaingia nyavuni....
Hartbreak: City keeper Joe Hart is powerless to prevent Siem De Jong's opener, leaving Gael Clichy and Pablo Zabaleta aghast (below)City keeper Joe Hart hoi...


MALAGA
Klabu inayoshiriki kwa mara ya kwanza, Malaga, imefuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 baada ya kutoka sare ugenini ya 1-1 na AC Milan na kusaidiwa na matokeo ya Mechi nyingine ya Kundi hili ambapo Anderlecht waliitungua Zenit St Petersburg bao 1-0.Bao la Malaga lilifungwa Kipindi cha Kwanza na Mchezaji wa Ureno Eliseu na AC Milan kusawazisha kwa bao la Mbrazil Alexandre Pato kaika Dakika ya 73 Uwanjani San Siro.

REAL MADRID 2  vs  BORUSSIA DORTMUND 2
Wakiwa wanajitayarisha kushereherekea kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mabingwa wa Germany, Borussia Dortmund, waliokuwa wakiongoza 2-1 ndani ya Santiago Bernabeu waliruhusu frikiki ya Real Madrid katika Dakika ya 89 ya Mesut Ozil kutinga wavuni na gemu kumalizika kwa sare ya 2-2 na hivyo kuiweka pembeni kwa muda ndoto yao ya kusonga.
Hadi mapumziko, Dortmund walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-1 yaliyofungwa na Marco Reus na Alvaro Arbeloa, aliejifunga mwenyewe, na Pepe kuifungia Real Madrid.


RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku Bongo Taimu]
Jumatano Novemba 7
Juventus v FC Nordsjælland
Chelsea FC v FC Shakhtar Donetsk
Valencia CF v FC BATE Borisov
FC Bayern München v LOSC Lille
SL Benfica v FC Spartak Moskva
Celtic FC v FC Barcelona
CFR 1907 Cluj v Galatasaray A.S.
SC Braga v Manchester United FC

No comments:

Post a Comment