
Kipa Bara, Juma Kaseja (kushoto) akiokoa moja ya hatari mbele ya mshambuliaji wa Zanzibar, Khamisi Mcha ‘Vialli’katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole Kampala leo. Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120, Bara wakitangulia kupata bao kupitia kwa Mwinyi Kazimoto dakika ya 10 kabla ya Abdallah Othman Ali kuisawazishia Zanzibar dakika ya 85.

Beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Haroub Nadir akimzuia mshambuliaji wa timu ya Zanzibar Heroes, John Boko wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda

Mchezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,Athuman Chuji akimtoka beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Sabri Aliy Makame wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda

Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, John Boko akiwatoka mabeki wa timu ya Zanzibar Heroes wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
Picha kwa hisani ya Shafi dauda
No comments:
Post a Comment