Geoffrey ‘Baba’ Kizito na Robert Ssentongo ndio waliokuwa wafungaji wa mabao hayo.
The Cranes sasa itakutana na Kilimanjaro Stars ambayo ilitinga nusu fainali baada ya kuichapa timu ya taifa ya Rwanda Amavubi kwa mabao nusu fainali itakayopigwa jioni ya alhamisi.

Kenya imeungana na timu za taifa za
Zanzibar na Kilimanjaro Stars kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano
ya Cecafa Tusker Cup 2012 baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0
dhidi ya timu ya taifa ya Malawi ambao walikuwa ni waalikwa katika
michuano ya mwaka huu mchezo uliopigwa katika dimba la Mandela lililoko
katika kitongoji cha Namboole.

Mike Barasa ndiye aliyefunga bao pekee la washindi ambalo limeifanikisha Harambe Stars kutinga nusu fainali ua michuano hiyo ya 34 ambayo ni mikongwe kuliko yote barani Afrika.
Harambe Stars sasa itakutana na mabingwa wa mwaka 1995 Zanzibar ambao wamewaondosha Burundi mabao 6-5 kwa njia ya penati katika hatua ya robo fainali.

Final Group A standings
- Uganda - 9 points
- Kenya - 6 points
- Ethiopia - 3 points
- South Sudan - 0 points
No comments:
Post a Comment