
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margreth Natongo Zziwa akifungua rasmi mashindano ya mpira wa miguu na mikono kwa wabunge wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mashindano haya ambayo hafanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya Tanzania, Kenya, Uganda, Bunrundi, Rwanda pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Bururndi haikushiri. Mwaka huu mashindono yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya. Spika Natongo Zziwa amewashukuru Maspika wote ambao wameziwezesha nchi zao kushiriki mashindano haya.

Maandamano ya uzinduzi

Kikosi cha Tanzania wakati wa uzinduzi.

Kikosi cha Uganda: Baada ya uzinduzi timu ya Bunge la Uganda na timu ya Bunge la Afrika Mashariki ndizo zilizofungua dimba ambapo zilitoka sare ya bao moja kwa moja. Mechi itakayofuata ni kati ya Tanzania na Kenya.

Kikosi cha Afrika Mashariki

Kikosi cha Tanzania kikiusoma mchezo kati ya Uganda na Afrika Mashariki
Wa TZ

Muamuzi wa mchezo huo Bi Damaris Kimani kutoka Kenya.
Na Prosper Minja-Bunge
No comments:
Post a Comment