Afrika Kusini, wenyeji wa
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, imefuzu kucheza hatua
ya robo fainali baada ya kutoka sare ya 2-2 na Morocco.
Kwa matokeo hayo Afrika Kusini inaongoza kundi A ikiwa na pointi 5 sawa na Cape Verde, lakini ikiizidi kwa wingi wa magoli.Katika mchezo wa leo Morocco ndiyo iliyoanza kufunga katika dakika ya kumi ya mchezo, likitiwa kimiani na El Adoua.
Matokeo hayo yaliyodumu hadi mapumziko.
Morocco haikukata tamaa kusaka ushindi, na iliwezakutia kimiani goli la pili katika dakika ya 82, mfungaji akiwa Abdelilah Elhafidi.
Furaha ya Morocco ilidumu kwa dakika nne tu, kwani katika dakika ya 86, Afrika Kusini kupitia kwa mshambuliaji wake Rantie, walisawazisha na kukata tikiti ya kucheza robo fainali.
Afrika Kusini na Cape Verde ndizo zilizofuzu katika kundi A kucheza hatua ya robo fainali.
Kundi B kesho litakuwa linakamilisha michezo yake, kwa Ghana kumenyana na Niger, huku DR Congo ikipepetana na Mali.Mpaka sasa Ghana ndiyo inayoongoza kundi hilo ikiwa na pointi 4, ikifuatiwa na Mali pointi 3, DR Congo pointi 2 na Niger imeweka kibindoni pointi 1.
Morocco wakitupia goli nyavuni
Kwenye Robo Fainali, Afrika Kusini watacheza na Mshindi wa Pili wa KUNDI B na Cape Verde watamvaa Mshindi wa KUNDI B.
Kesho Jumatatu KUNDI B linamaliza Mechi
zake kwa Mechi kati ya Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2
Usiku] na Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku].
MSIMAMO:
KUNDI A
1 South Africa Mechi 3 Pointi 5
2 Cape Verde Mechi 3 Pointi 5
3 Morocco Mechi 3 Pointi 3
4 Angola Mechi 3 Pointi 1
KUNDI B
1 Ghana Mechi 2 Pointi 4
2 Mali Mechi 2 Pointi 3
3 Congo DR Mechi 2 Pointi 2
4 Niger Mechi 2 Pointi 1
KUNDI C
1 Burkina Faso Mechi 2 Pointi 4
2 Nigeria Mechi 2 Pointi 2
3 Zambia Mechi 2 Pointi 2
4 Ethiopia Mechi 2 Pointi 1
KUNDI D
1 Ivory Coast Mechi 2 Pointi 6
2 Tunisia Mechi 2 Pointi 3
3 Togo Mechi 2 Pointi 3
4 Algeria Mechi 2 Pointi 0
No comments:
Post a Comment