Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria. Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo .
Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.
Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.
Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.
No comments:
Post a Comment