BUKOBA SPORTS

Monday, January 28, 2013

CHRISTIANO RONALDO ATUPIA HAT-TRICK YA 19 KWA REAL MADRID TANGU AJIUNGE NAO 2010, LIONEL MESSI AKICHINJA 4. EL CLASSICO KUTEGUA KITENDAWILI KIGUMU JUMATANO HII!!!


Ronaldo akifunga penalti wakati wa mechi yao dhidi ya Getafe jana.

Messi akifunga goli lake la nne na la tano kwa Barcelona dhidi ya Osasuna jana

Mesut Ozil (kulia) wa Real Madrid akishangilia na Cristiano Ronaldo baada ya Ronaldo kufunga goli la pili la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013. Real walishinda 4-0.

Mesut Ozil (kulia) wa Real Madrid akishangilia na Cristiano Ronaldo baada ya Ronaldo kufunga goli la pili la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013.

Mesut Ozil (kulia) wa Real Madrid akishangilia na Cristiano Ronaldo baada ya Ronaldo kufunga goli la pili la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013.

Mesut Ozil (kulia) wa Real Madrid akishangilia na Cristiano Ronaldo baada ya Ronaldo kufunga goli la pili la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013.

Napita humu... Cristiano Ronaldo (Namba 7) wa Real Madrid akichungwa na Juan Valera wa Getafe wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013.

Cristiano Ronaldo (katikati) wa Real Madrid akifunga goli la tatu la Real wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Getafe kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013.

Cristiano Ronaldo (kushoto) wa Real Madrid akipiga mpira mbele ya Alexis Ruano na Juan Valera wa Getafe wakati wa mechi yao ya La Liga kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid, Hispania Januari 27, 2013.

Messi akikatiza

Lionel Messi (kushoto) wa FC Barcelona akishangilia na Puyol baada ya kufunga goli la pili la timu yake kwa njia ya penalti wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona Hispania Januari 27, 2013. Barca walishinda 5-1

Lionel Messi wa FC Barcelona akifunga goli la pili la timu yake kwa njia ya penalti wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona Hispania Januari 27, 2013. Barca walishinda 5-1

Lionel Messi wa FC Barcelona akimpiga chenga kipa wa Osasuna (aliyekaa chini) na kufunga goli la kuongoza la timu yake wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona Hispania Januari 27, 2013.
Lionel Messi (kushoto) wa FC Barcelona akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la kuongoza wakati wa mechi yao ya La Liga dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona Hispania Januari 27, 2013.
Lionel Messi akipita katikati ya wachezaji wa Osasuna
MECHI ya El Classico ya nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme baina Real Madrid na Barcelona kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumatano itakuwa ni balaa kufuatia matokeo ya jana timu hizo mbili kubwa Hispania.

Real Madrid waliianza siku ya Jumapili mapema kwa ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Getafe, ambayo kwa mara nyingine tena ilishuhudia Cristiano Ronaldo akiwa katika kiwango chake cha juu kabisa cha kufunga mabao.

Ronaldo alifunga 'hat trick' dhidi ya mahasimu wao wa mji wa Madrid huku magoli yote matatu yakija katika kipindi cha pili.
Ulikuwa ni ukurasa mwingine wa msimu mzuri kwa Mreno huyo. Na namna ambayo Ronaldo alifunga 'hat trick' hiyo ni lazima pia izingatiwe: Goli moja alifunga kwa mguu wa kushoto, jingine mguu wa kulia na la tatu kwa kichwa. 'Hat trick' iliyokamilika kabisa kama ilikuwapo nyingine kama hiyo.

Magoli yote matatu ya Ronaldo yalikuja ndani ya dakika 10 tu na ilikuwa ni 'hat trick' yake ya 20 maishani na ya 19 akiwa na Real Madrid.

Idadi hiyo inafanya sasa Ronaldo awe amefunga jumla ya magoli 179 katika mechi 176 tangu alipotua misimu mitatu na nusu iliyopita akitokea Manchester United na imemuweka katika Na.6 ya wafungaji vinara wa zama zote klabuni hapo akiwa amemfikia gwiji wa zamani Francisco Gento. Kwa magoli 10 ambayo tayari ameyafunga mwaka huu pekee wa 2013, Ronaldo yuko katika kasi ya kuyafikia magoli ambayo Lionel Messi alifunga mwaka 2012 na kuvunja rekodi.

Lakini walisema kila Ronaldo analolifanya, Messi hulifanya vizuri zaidi na ilikuwa hivyo pia jana.

Messi jana aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya La Liga kufunga katika mechi 11 mfululizo wakati alipofunga magoli manne katika ushindi wa Barcelona wa 5-1 dhidi ya Osasuna kwenye Uwanja wa Nou Camp baadaye jana.

Muargentina huyo sasa amefikisha magoli 33 katika mbio za kuwania tuzo ya 'Pichichi' ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Hispania akifuatiwa na Ronaldo aliyefikisha magoli 22 baada ya 'hat trick' yake dhidi ya Getafe.


Messi sasa amefikisha jumla ya mabao 202 katika La Liga na kuwa mmoja wa wachezaji saba tu waliovuka magoli 200 katika Ligi Kuu ya Hispania.

Osasuna inaonekana kuwa ni timu ambayo Messi "anapenda" kuifunga baada ya kifunga jumla ya magoli 14 katika mechi 13 aliziocheza dhidi yao.

Hii ni mara ya tatu kwa Messi kufunga magoli manne katika mechi moja ya ligi, mara nyingine mbili zikija katika msimu wa kipekee kwake, alipofunga dhidi ya Valencia na Espanyol.


HISTORIA YA HAT-TRICK ZAKE REAL.
Date - Opponent, competition, minutes of goals (full time score) time between first and last goal

2009-2010
May 5 - Malaga (A) League 26, 56, 72 (won 4-1) 46min
2010-2011
October 23 - Racing Santander (H) League 15, 27, 47, pen 55 (won 6-1) 32min (last three 28min)
November 20 - Athletic Bilbao (H) League 30, 62, pen 90 (won 5-1) 60min
December 22 - Levante (H) Copa del Rey 45, 72, 74 (won 8-0) 29min
January 9 - Villarreal (H) League 9, 45, 79 (won 4-2) 70min
March 7 - Malaga (H) League 51, pen 68, 77 (won 7-0) 26min
May 7 - Sevilla (A) League 31, 65, 70, 75 (won 6-2) 39min (last three in 10min)
May 10 - Getafe (H) League 24, 58, pen 90 (won 4-0) 66min

2011-2012
August 28 - Zaragoza (A) League 24, 71, 87 (won 6-0) 63min
September 24 - Rayo Vallecano (H) 39, pen 51, pen 84 (won 6-2) 45min
October 22 - Malaga (A) 23, 28, 38 (won 4-0) 15min
November 6 - Osasuna (H) 23, pen 54, 58 (won 7-1) 35min
December 17 - Sevilla (A) 10, 41, pen 85 (won 6-2) 75min
February 12 - Levante (H) pen 45, 50, 57 (won 4-2) 12min
April 11 - Atletico Madrid (A) 25, 68, pen 83 (won 4-1) 58min

2012-2013September 30 - Deportivo La Coruna (H) pen 23, 44, pen 84 (won 5-1) 61min
October 3 - Ajax (A) Champions League 42, 79, 81 (won 4-1) 41min
January 9 - Celta Vigo (H) Copa del Rey 3, 24, 87 (won 4-0) 84min
January 27 - Getafe (H) League 62, 65, pen 72 (won 4-0) 10min

No comments:

Post a Comment