BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 29, 2013

DAVID BECKHAM YU' GUNNERS KUFANYA MAZOEZI, WENGER HANA NIA YA KUMSAJILI GWIJI HUYO!!

Kiungo na Nahodha wa zamani wa England David Beckham amekuwa akifanya mazoezi na Timu ya Arsenal kama ilivyothibitishwa na Meneja wa Timu hiyo Arsene Wenger ambae, hata hivyo, amekanusha habari za kutaka kumsaini Mkongwe huyo.
Wenger amesema Beckham aliwasiliana nae akiomba kujiweka fiti na akamkubalia.
Hivi sasa Beckham hana Klabu yeyote baada ya kung’atuka kuichezea Los Angeles Galaxy inayocheza Ligi ya MLS huko USA mwishoni mwa Mwaka jana.
Beckham alijitengenezea jina lake alipokuwa na Manchester United na baadaye kuichezea Real Madrid na pia AC Milan.
Kwa sasa Beckham ana Umri wa Miaka 37Beckham akifanya mazoezi na wachezaji wa Arsenal

No comments:

Post a Comment