Mario Balotelli
Balotelli, 22, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu mjini Milan siku ya Jumatano kabla ya kusaini wake na klabu hiyo.
Inakisiwa kuwa AC Milan imemsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 20.
Awali Manchester City ilianzisha mazungumzo na vilabu vya AC Milan na Juventus kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake Mario Balotelli, na ripoti zinasema kuwa, Balotelli atauzwa ikiwa vilabu hivyo vitaweza kulipa fedha wanazo taka.
Klabu hiyo imesema mchezji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakisiwa kugharibu pauni milioni ishirini na moja mbali na fedha zingine za ziada.
Kinyume na matarajio ya wengi Balotelli amesafiri na wachezaji wa Manchester City watakaocheza na QPR katika mechi ya ligi kuu ya premir leo usiku.Milan ilianzisha mazungumzo na Man City, kuhusu mchezaji huyo kutoka Italia na kuna ripoti kuwa klabu ya Juventus vile vile imewasilisha ombi la kutka kumsajili Balotelli, ambaye alijiunga na Manchester City Agosti mwaka wa 2010 kwa kitita cha pauni milioni 24.
CITY IN THE PREMIER LEAGUE
BALOTELLI IN ALL COMPETITIONS
No comments:
Post a Comment