BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 29, 2013

HATIMAYE MSANII ELIZABERTH MICHAEL APATA DHAMANA LEO KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU, MAMA YAKE AMPOKEA KWA FURAHA NA HUKU MACHOZI YAKIMTIRIRIKA!!!, LULU AWASHUKURU WALIOMPATIA MDHAMANA, SASA KUONEKANA URAIANI.

Elizabeth Michael (Lulu)
MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama. Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na furaha mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.
Baadaye, mama huyo alionekana kujawa na hisia kali kiasi cha kumwaga machozi yatokanayo na furaha aliyokuwa nayo baada ya mahakama kumuachia binti yake kwa dhamana na wote wawili kuonekana wakikumbatiana; kama watu wasioamini juu ya kile kilichotokea.

No comments:

Post a Comment