VINARA Manchester United wameishinda 2-1 Southampton Uwanjani Old Trafford na kukwea Pointi 7 mbele kileleni ligi kuu England, Barclays Premier League,United ndiyo walianzwa kufungwa goli la kizembe mwanzoni dakika ya 3 kupitia mchezaji Jay Rodriguez baada ya kumpita kipa De Gea kwa makosa ya beki kurudisha mpira mbovu nyuma kwa kipa.
Goli la kusawazisha kwa Manchester United lilifungwa na mshambuliaji Rooney dakika ya 8 na goli la ushindi likafungwa tena na Wayne Rooney dakika ya 27.
Kipindi cha pili hakuna aliyeweza kuziona nyavu za mwenzake Pamoja na United kuelemewa na Southampton muda mwingi wa kipindi cha pili. United inaongoza ligi hiyo kwa ponti 59 yenye wapenzi wengi Duniani kwa pointi 7 mbele ya Man City yenye pointi 52.
Evra akipiga kichwa kugawa mpira kwa Rooney
Rooney akipokea pasi kutoka kwa Evra
mpira ukidondoka nyuma ya nyavu za Southampton
Danny Welbeck akitaka kukatiza kwa Morgan Schneiderlin (kulia) na hatimaye kuzuiliwa
Rooney akipokonywa mpira na kipa Soton wakati anataka kufunga goli la tatu usiku
VIKOSI:
Man Utd: De Gea, Jones, Smalling (Ferdinand 63), Vidic, Evra, Welbeck, Carrick, Anderson (Rafael 68), Kagawa (Nani 73), Rooney, van Persie.
Subs not used: Lindegaard, Valencia, Cleverley, Buttner.
Goals: Rooney 8, 27
Booked: Vidic, Rafael
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Fox (Shaw 78), Schneiderlin, Cork, Puncheon (Steven Davis 46), Rodriguez, Ramirez (Lallana 46), Lambert.
Subs not used: Kelvin Davis, Lee, Richardson, Chaplow.
Goals: Rodriguez 3
Booked: Schneiderlin
Referee: Lee Mason (Lancashire)
Attendance: 75,600
RATIBA MECHI ZIJAZO
Jumamosi Februari 2
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
QPR v Norwich
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Stoke
Everton v Aston Villa
Newcastle v Chelsea
Reading v Sunderland
West Ham v Swansea
Wigan v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Fulham v Man United
Jumapili Februari 3
[SAA 10 na Nusu Jioni]
West Brom v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
Man City v Liverpool
No comments:
Post a Comment