BUKOBA SPORTS

Saturday, January 26, 2013

FA CUP: ASTON VILLA YATUPWA NJE NA MAYOSO "MILLWALL" YACHAPWA 2-1. KOCHA WA VILLA ASEMA WANA BAHATI MBAYA !!

Aston Villa imejikuta ikibwagwa nje ya Vikombe vikubwa na Timu za Madaraja ya chini baada ya kutolewa nje ya FA CUP na Timu ya Daraja la chini Millwall kwa kufungwa bao 2-1 katika Mechi ya Raundi ya 4.
Ni bao la Dakika ya 89 la John Marquis ambalo limewatupa Aston Villa nje na kipigo hiki kinafuatia Juzi Jumanne kutolewa kwenye CAPITAL ONE CUP na Bradford City kwenye Nusu Fainali.
Hali ya Aston Villa kwenye Ligi Kuu England pia so shwari na wako nafasi ya 17, ikiwa ni nafasi moja tu juu ya zile Timu 3 za mkiani ambazo mwisho wa Msimu hushushwa Daraja.

Mashabiki wa Millwall walimtupia pia refa mshika kibendelea chupa
Mhhh....hii ni chupa ya maji,bia, au....

Refa naye alijionea chupa live iliyotupwa uwanjani hapo.

Chupa ikimkosa kosa Charles N'Zogbia wakati anasubilia kupiga frii kiki usiku iliyotupwa na shabiki

Millwall....Goli...

Darren Bentakiipatia timu yake ya Aston Villa goli dakika ya 22

Danny Shittu akitupia kuipa ushindi Millwall

Shittu (kulia) akishangilia baada ya kufunga goli.

Maneja wa Villa Paul Lambert akikosa nafasi ya kushinda vikombe ndani ya siku nne na huku akijionea kipigo kwa timu yake.

VIKOSI:
Millwall: Forde, Adam Smith, Shittu, Osborne, Beevers, Henry, Trotter, Abdou, Feeney, Marquis (Jack Smith 90), Keogh (N'Guessan 82). Subs Not Used: Maik Taylor, Dunne, Wright, Batt, Wilkinson.
Booked: Beevers.
Goals: Shittu 27, Marquis 89.
Aston Villa: Given, Vlaar, Clark, Lichaj, Lowton, Westwood, Delph (Bannan 39), N'Zogbia, Bennett, Bent, Weimann (Bowery 81). Subs Not Used: Guzan, Ireland, Agbonlahor, Holman, Williams.
Booked: Bennett, Bowery.
Goals: Bent 22.
Att: 15,007
Ref: Neil Swarbrick


FA CUP
RAUNDI YA 4
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Januari 25
Millwall 2 Aston Villa 1
Jumamosi Januari 26
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Stoke City v Manchester City
[SAA 12 Jioni]
Norwich City v Luton Town
Macclesfield Town v Wigan Athletic
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Brighton & Hove Albion v Arsenal
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR v MK Dons
Bolton v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Manchester United v Fulham

Jumapili Januari 27
[SAA 9 Mchana]
Brentford v Chelsea
[SAA 11 Jioni]
Leeds United v Tottenham Hotspur
[SAA 1 Usiku]
Oldham Athletic v Liverpool

No comments:

Post a Comment